Black Sheep

Black Sheep
Dres (left) & Mista Lawnge (right)
Dres (left) & Mista Lawnge (right)
Maelezo ya awali
Asili yake Queens/Brooklyn, New York, Marekani
Miaka ya kazi 1989–1995
2000–
Studio Mercury/PolyGram/Universal
Ame/Wameshirikiana na Showbiz and A.G.
Chi Ali
Native Tongues
The Legion
Wanachama wa sasa
Dres
Mista Lawnge


Black Sheep ni kundi la hip hop linalounganishwa na wasanii wawili kutoka mjini Queens, New York. Ndani yake anakuja Andres "Dres" Titus na William "Mista Lawnge" McLean. Wawili hawa wanatokea mjini New York, lakini walikutana wakati wakiwa vijana huko mjini North Carolina, ambapo familia zao zilihamia huko.[1]

Kundi lilikuwa na uhusiano na Native Tongues, ambamo wakiwa pamoja na Jungle Brothers, A Tribe Called Quest, na De La Soul. Baada ya kuwa pamoja kunako 1989, Black Sheep wakatoa albamu yao ya kwanza mnamo 1991 wakiwa na kibao chao kikali cha "Flavor of the Month" na baadaye kutoa albamu ya kwanza ya A Wolf in Sheep's Clothing, ambapo iliwapatia sifa na umaarufu wa kina katika jumuia nzima ya hip-hop kwa mashairi na albamu yao isio na kifani.

Baada ya miaka sita ya kuwa pamoja, Black Sheep wakatengana mnamo 1995, lakini wakaamua kuungana tena baada ya miaka 5.

  1. Bush, John. [Black Sheep katika Allmusic "Black Sheep: Biography"]. allmusic. Iliwekwa mnamo 2009-08-03. {{cite web}}: Check |url= value (help)

From Wikipedia, the free encyclopedia · View on Wikipedia

Developed by razib.in